Ninaweza kuwa nani? Taaluma za STUH/STEM kutoka A-Z ni kitabu cha
picha za kialfabeti cha kumotisha na rahisi kusoma kinachofundisha
kizazi chetu kijacho kuhusu taaluma za Sayansi, Teknolojia,
uhandisi na Hisabati.Kitabu hiki kinatoa vielelezo vyenye rangi vya
watoto sita tofauti wanaowakilisha taaluma mbalimbali za STUH/STEM
(kwa mfano, wanaanga, madaktari, wanasayansi,na wahandisi, na
kadhalika), kuwasaidia watoto(miaka 5 hadi 8) kujiona katika
mojawapo ya taaluma za STUH/STEM, na kuwapa motisha ya kuandaa
maisha yao ya baadaye kupitia STUH/STEM!